Nakala asilia kwa Kiingereza na Tactical Tech, tafsiri na marekebisho na washirika:
Ndani ya moduli hii, utaangazia taarifa potovu —mwonekano wake, namna inavyoenezwa, na namna unavyoweza kuishughulikia, huku ukijikita katika tabia na mienendo iwezayo kukuweka salama. Pia utaangazia namna teknolojia hutumika kushawishi hisia zako, mtazamo wako na imani yako, na jambo unaloweza kufanya kuhusu hilo.
Imarisha utambuzi wako binafsi linapokuja suala la utafiti, ukusanyaji na usambazaji wa taarifa, jifunze kuhusu Kanuni ya Kutosababisha Madhara, na namna ya kupunguza hatari kwako na kwa jamii yako.
Fahamu aina tofauti za taarifa potovu na tambua viwango vya athari.
Chunguza jinsi na sababu za uchaguzi wa chapisho zilizopo kwenye mpasho wako wa habari, na amua kama unaweza kuiamini taarifa iliyopo kwenye mpasho wako.
Tambua chambo ya kubofya na vyanzo visivyoaminika, funza macho yako kutambua anuani za kilaghai za wavuti, na jifahamishe kuhusiana na vifuatiliaji.
Tambua “cheap fakes” and “deepfakes”—zinaweza zisiwe za kutambulika kirahisi kama unavyofikiria.
Fanya jaribio fupi kupima kile ulichojifunza katika kipindi cha moduli ya kwanza ya Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer Kit).