Nakala asilia kwa Kiingereza na Tactical Tech, tafsiri na marekebisho na washirika:
Kama utavyokumbuka kutoka Moduli ya 1, kazi yako kama Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer) inahitaji mageuzi ya mtazamo wa kifikra. Pia, ulijifunza kwamba suala la utofautishaji ukweli na uwongo mtandaoni linaweza kuwa gumu. Sasa, u tayari kuingia kwenye hatua inayofuata: utafiti na uhakiki wa taarifa za mtandaoni.
Moja ya njia madhubuti zaidi ya kufanya utafiti ni kufuata Njia ya Kisayansi. Kama jina lenyewe linavyojieleza, wanasayansi waliopo ndani ya maabara, watafiti wa taaluma nyingine mbalimbali, pamoja na wataalamu kutoka nje ya wigo wa kisayansi, hufuata hatua hizi.
Kabla ya kuingia kwenye utafiti wako, huu ni muda muafaka kwako kutathmini namna unavyojilinda wewe na vifaa vyako katika msingi wa shughuli za kila siku.
Somo hili litakusaidia kuwa mpekuzi mkali zaidi wa vyanzo vya taarifa na kuweza kujifunza nini kinafanya chanzo fulani kuwa cha kuaminika.
Somo hili litakusaidia kutofautisha aliye halisi na yule asiye.
Katika somo hili, utaangazia tafuzi wa ugeuzi wa picha na upataji wa chimbuko la picha.
Ndani ya somo hili, yote yaliyomo humu yatahusisha suala la muda—kile tarehe ya uchapishaji pekee inaweza kubainisha, na vidokezo vya kutafuta.
Fanya jaribio fupi kupima kile ulichojifunza katika kipindi cha moduli ya kwanza ya Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer Kit).
DFRLab, EUvsDisinfo, Oxford Internet Institute, The Information Operation Archive
The Global Investigative Journalism Network: COVID-19 resources
Poynter Institute’s International Fact-Checking Network