Nakala asilia kwa Kiingereza na Tactical Tech, tafsiri na marekebisho na washirika:
Katika somo hili, utachunguza jinsi ya kukusanya na kuandika mchakato wako wa utafiti na matokeo kwa uangalifu. Utapata pia jinsi ya kuanzisha timu na vidokezo vya kushirikiana kwa usalama.
Hapa utabaini mpango wako wa usalama. Kila udadisi wa kidigitali (digital enquiry) huwa na mahitaji na hatari zake za kipekee, zinazohitajika kukadiriwa na kuwekewa mpango. Eneo zuri la kuanzia ni kujifunza namna ya kusikiliza na kufuata dhamiri na hisia zako, na kisha kujenga juu ya msingi huo.
Hapa, utajifunza kuhusu ushirikiano wa kikazi kwenye muktadha wa kazi yako kama Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer) na kuangazia namna za kukusaidia wewe na kundi lako kufikia malengo yenu.
Hapa utajifunza jinsi ya kuchagua zana shirikishi sahihi kwa ajili ya kazi yako, kama Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer), na ndani ya mazingira ya kundi.
Hapa utajifunza kuhusu namna ya kuhifadhi kumbukumbu za udadisi wako wa kidigitali (digital enquiry), kuanzia taarifa gani za kujumuisha hadi katika suluhisho za uhifadhi za kukuweka wewe, utafiti wako, na watu wako wa karibu, salama.
Hapa, utajizatiti katika uhifadhi nyaraka za udadisi wako w a kidigitali (digital enquiry) kwa uangalifu na kwa kuzingatia usalama.
Pima ufahamu wako kupitia maswali haya kumi ya haraka, yahusuyo uhifadhi wa nyaraka na ushirikiano wa pamoja kwenye udadisi wako wa kidigitali (digital enquiry).