- Sehemu ya 1
Kutambua na Kujibu Taarifa Potovu
Ndani ya moduli hii, utaangazia taarifa potovu —mwonekano wake, namna inavyoenezwa, na namna unavyoweza kuishughulikia, huku ukijikita katika tabia na mienendo iwezayo kukuweka salama. Pia utaangazia namna teknolojia hutumika kushawishi hisia zako, mtazamo wako na imani yako, na jambo unaloweza kufanya kuhusu hilo.
- Sehemu ya 2
Uhakiki wa Taarifa za Mtandaoni
Kama utavyokumbuka kutoka Moduli ya 1, kazi yako kama Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer) inahitaji mageuzi ya mtazamo wa kifikra. Pia, ulijifunza kwamba suala la utofautishaji ukweli na uwongo mtandaoni linaweza kuwa gumu. Sasa, u tayari kuingia kwenye hatua inayofuata: utafiti na uhakiki wa taarifa za mtandaoni.
Katika somo hili, utachunguza jinsi ya kukusanya na kuandika mchakato wako wa utafiti na matokeo kwa uangalifu. Utapata pia jinsi ya kuanzisha timu na vidokezo vya kushirikiana kwa usalama.